Mchakato umekamilika, mabilionea hawa kuinunua Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kampuni ya Jackson Group iliyopewa tenda ya kuchakata na kuithaminisha (kujua thamani) ya Klabu ya Yanga imekamilisha kazi hiyo.


Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, muda wowote klabu hiyo inatarajia kutangaza thamani ya klabu yao. Pia, itatangaza rasmi jinsi yaa uuzwaji wa hisa.


Ma-millionaire kadhaa tayari wameonesha nia ya kununua hisa hizo wakiwemo;


◉ Rostam Aziz ◉ Ghalib Said Mohammed (GSM) ◉ na wengine kadhaa.


Mchakato wa uuzaji wa hisa ukikamilika Yanga itakuwa klabu ya kwanza Tanzania kukamilisha mchakato wa mabadiliko.


Baada ya kila kitu kukamilika muundo wa klabu ya Yanga SC utakuwa hivi ;


◉ Young Africans sports club itaendelea kubaki chini ya mkutano mkuu General assembly) , Baraza la wadhamini, wajumbe wa kamati ya utendaji na wanachama.


◉ Young Africans sports club itafungua KAMPUNI ambayo yenyewe itamiliki 51% za hisa zote na kuwaachia wawekezaji 49% za hisa zilizobaki 'REMAINING SHARES'.


◉ Kampuni hii mpya kazi yake itakuwa ni kuendesha shughuli za mpira na BIASHARA za mpira pekee kwa niaba ya Yanga SC


◉ Kampuni hiyo itakuwa na uongozi wake ambao ni BODI ya WAKURUGENZI ambao watamuajiri mtendaji mkuu (CEO) ambaye yeye naye ataajiri watendaji wote chini yake wakumsaidia kuendesha hii kampuni kama TAASISI ya mpira.


◉ Kwenye bodi ya wakurugenzi itayoanzishwa kusimamia kampuni hiyo kutakuwa na jumla ya wajumbe (9) wa bodi, Yanga SC itatoa wajumbe (5) na WAWEKEZAJI kwa UJUMLA wao watatoa wajumbe (4).


◉ Nafasi moja ya ujumbe kwenye bodi itapatikana kwa kununua (12.5%) ya hisa, hivyo ili muwekezaji apate nafasi kwenye bodi lazima anunue angalau asilimia hizo za hisa kuingia kwenye bodi.


Ni lazima kuwe na wawekezaji zaidi ya mmoja watakaonunua 49% ya hisa na wasiozidi wanne, muundo haukubali Muwekezaji mmoja.


Yanga itakuwa klabu yenye thamani kubwa zaidi Afrika mashariki ikifuatiwa na Simba SC yenye thamani ya Tsh bilioni 20.

Usikose kutazama mechi zote za ligi kuu TZ bara, ulaya na nyingine kibao live bure kabisa pakua app yetu kutazama Sasa bofya hapa kudownload

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post