Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Katika tuzo ya mchezaji bora wa msimu huo (MVP), likachomoza jina la Maxi Mpia Nzengeli aliyekuwa akiitumikia AS Maniema Union wakati huo akiwa na umri wa miaka 21 tu
Msimu uliopita Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alifanya jitihada kumsajili Maxi lakini haikuwa rahisi AS Maniema kumuachia nahodha wao huyo. Hersi hakukata tamaa, msimu huu akajaribu tena na hatimaye amefanikiwa kumleta Maxi ndani ya klabu ya Yanga
Kocha wa AS Vita Raul Shungu ambaye amewahi kuifundisha Yanga mwaka 1998, amesifu usajili wa mchezaji huyo akiwahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa watarajie mambo makubwa kutoka kwake
"Nimeona Yanga wamemsajili Maxi, huyu ni mchezaji mwingine bora kabisa amekuja hapa Tanzania, naweza kusema kama ni kitabu basi Maxi ni toleo jipya badala ya Fiston (Mayele),” alisema Shungu ambaye kikosi chake kiko Tanzania kikifanya pre-season
"Nilizungumza wakati ule Mayele anafika hapa tena kabla ya kuanza kucheza. Nilisema ni mchezaji bora ambaye kama ataweka juhudi atasumbua sana na ikawa hivyo, nafikiri mliona wote sasa vilevile timu pinzani zimchunge huyu Maxi”
"Kipaji chake ni kikubwa sana anaweza kucheza nafasi nyingi uwanjani, ana nguvu, kasi na kitu kizuri zaidi kwa Yanga watafaidi kwa kuwa ni kijana mdogo atawasaidia sana mtamuona pia akifunga sana," Shungu alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
Ukweli wa maneno ya Shungu ulianza kuonekana kwenye mchezo wa wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, Maxi akicheza kwa dakika 45 ambazo zilitosha kumtambulisha kwenye soka la Tanzania
Post a Comment