Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mkono mwingine unapigwa na Wananchi katika uwanja wa Azam Complex, Yanga ikitinga raundi ya kwanza ligi ya mabingwa kibabe kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Asas Fc ya Djibout
Yanga inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 na sasa itacheza na El Merrikh katika mchezo wa raundi ya kwanza
Ilikuwa ni Maxi Day, ama kwa hakika imekuwa siku njema kwa Maxi Nzengeli kwani aliitendea haki siku hii
Maxi alifunga mabao mawili katika mchezo huo ambao ilitawala kwa muda wote
Mabao mengine yalifungwa na Hafiz Konkoni, Pacome Zouzou na Clement Mzize
Yanga inafunga mabao matano katika mchezo wa pili mfululizo, ikitoka kuibugiza KMC mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu
Post a Comment