Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ilikuwa siku maalum kwa mashabiki wa Simba kuishuhudia timu yao kwa mara ya kwanza baada ya maboresho
Kwa hakika dalili njema zimeonekana mapema, huu unaweza kuwa msimu bora kwa Wanamsimbazi
Willy Onana alihitaji dakika tano tu kuifungia Simba bao la kuongoza akipiga shuti lililomshinda mlinda lango kutoka nje kidogo ya 18
Simba ilitwala mchezo huo nyota wapya Onana na beki Che Malone Fondoh wakiwa kivutio kwenye kipindi cha kwanza
Bao la pili lilifungwa na yuleee namba sita, ambaye watu walipokwa uwanja wa ndege, Fabrice Ngoma
Ngoma alifanya uamuzi sahihi wa kutua Simba badala ya kule upande wa pili kwani jambo la uhakika ni kuwa msimu huu yuko kwenye kikosi bora na atashiriki mashindano makubwa 'Super League'
Ulikuwa mchezo ambao pengine Simba ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kwa idadi ya nafasi walizotengeneza
Luis Miquissone 'Konde Boy' kwa mara nyingine leo Wanasimba wamemuona baada ya kurejea
Alifanya majaribio kadhaa kwenye lango la Power Dynamos lakini haikuwa bahati kwake kuzifumania nyavu
Ilikuwa siku iliyojaa burudani kwa Wanasimba kuanzia asubuhi na kuhitimishwa kwa ushindi
Post a Comment