Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba imetinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Singida FG katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Mkwakwani
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana hivyo mshindi kuamuliwa kwa mikwaju ya penati
Luis Miquissone, Saido Ntibazonkiza, Mzamiru Yassin na Moses Phiri walifunga penati za Simba wakati Tchakei na Abuya walifunga kwa upande wa Singida FG huku Aziz Andambwile na Yusufu Kagoma wakikosa kwa upande wa Singida FG
Ni rasmi sasa Simba itachauana na Yanga kwenye mchezo wa fainali siku ya Jumapili wakati Azam Fc watachuana na Singida FG katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu
Post a Comment