Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa kushindwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya wapinzani wao Simba Sc.
Gamondi amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa katika dimba la CCM Mkwakwani Tanga jana Jumapili, Agosti 13, 2023 na Simba kuibuka mshindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-1 kufuatia kutoka sare ya bila kufungana katika dakika 90.
"Tulikamata mechi kwa dakika zote na tukacheza vizuri ila tukashindwa kupiga mipira langoni Simba walikuwa wanacheza mipira mirefu tu.
"Pia tulikuwa na nafasi nzuri ya kumaliza mechi kwenye penalties lakini bado tukashindwa tena. Tuna kikosi kizuri na nmeridhika nacho.
"Nimalize kwa kusema kuwa tunawaomba radhi mashabiki wa Yanga kwa kupoteza mchezo huu," amesema Gamondi.
Hii ni dabi ya kwanza ya Kariakoo kwa Kocha Gamondi ambaye ni raia wa Argentina huku ikiwa dabi ya pili ya Kocha Robertinho wa Simba ambaye katika michezo yote miwili amefanikiwa kushinda.
Post a Comment