Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Asas Fc
Kesho Jumamosi August 26, Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji angalau sare Ili kutinga raundi ya kwanza
Gamondi amesema anafahamu mchezo huo utakuwa tofauti na mchezo wa kwanza lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda na kusonga mbele
"Tuko tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Asas Fc. Tunafahamu utakuwa mchezo tofauti, wapinzani wetu watajaribu kutushambulia"
"Tutaingia kwenye mchezo huu pasipo kufikiria matokeo ya mchezo wa kwanza, tutahitaji kufunga mabao ili tusonge mbele," alisema Gamondi
Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Ushindi au matokeo yoyote ya sare yataihakikishia Yanga kusonga mbele raundi ya kwanza
Post a Comment