Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kwa Wanasimba, Simba Day ni kama sikukukuu, shughuli nyingine zote husimama ili kufurahia siku hii maalum
Simba Day leo itakuwa na ugeni mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi wa tukio hili
Mageti ya uwanja wa Benjamin Mkapa yatafunguliwa mapema tu ili kuwaruhusu mashabiki kuingia uwanjani kwa utaratibu mzuri
Tiketi zote zilishauzwa siku tatu zilizopita, Jeshi la Polisi limetahadharisha kama huna tiketi usiende uwanjani, baki nyumbani fuatilia kupitia Azam TV
Kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wakiongozwa na Ali Kiba, Tunda Man, Joh Makini, Meja Kunta na wengine kibao
Mechi za kirafiki kutoka timu ya Wanawake, timu ya vijana, wakongwe na matukio mengine ya kuwaburudisha Wanasimba
Simba Day leo itahitimishwa na matukio makubwa mawili; la kwanza ni utambulisho wa kikosi cha Simba cha msimu wa 2023/24
Ile shauku kubwa ya kumjua mlinda lango mpya aliyesajiliwa na Simba basi majibu yake ya majira yatapatikana saa 11 jioni
Pili kutakuwa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Power Dynamos, mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia
Tukio hili lipo mubashara kwenye app yetu kama hujaipakua bofya hapa kuipakua Bure kabisa
Post a Comment