Hata wakipeleka mechi kambi ya jeshi, Al-Merreikh tutawakanda tu - Kamwe

 Ally Kamwe.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Ofisa Habari wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema kuwa hata kama wapinzani wao wa Kimataifa, Al-Merreikh wakipeleka mechi yao nchini Ukraine au kwenye moja ya kambi zao za jeshi nchini SUdan, bado Yanga itashinda.


Kamwe amesema hayo mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya pili ya mtoano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo watakutana a na Merreikh ya Sudani ambayo imehamishia mechi zake nchini Morocco kutoka Rwanda kufuatia machafuko yaliyopo nchini mwao.


"Yanga bado hatujapata taarifa rasmi kama Al-Merreikh wamebadilisha uwanja, lakini kwa kikosi chetu cha sasa hivi, sio tu Morocco hata kama wangeipeleka hii mechi Ukraine kwenye mpaka ambapo kuna vita wakaomba tucheze nao, sisi tungewakanda vilevile.


"Level iliyofikia yanga haijali mechi tunakwenda kucheza wapi, tunajikita na dakika 90 tunakwenda kuchezaje. Kwa hiyo wasihangaike Al-Merreikh, hata wakienda Afghanistan, Iraq kokote hata Niger watuwekee tutawapiga tu.


"Wakina shida san ahata kwenye kambi yao ya jeshi pale Sudan ambapo kuna vita, waingie mle mle ndani halafu twende tukacheze nao, tutawapiga," amesema Ally Kamwe.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post