Gamondi akerwa na penati aliyosababisha Zawadi Mauya, "Sipendi kufungwa" - EDUSPORTSTZ

Latest

Gamondi akerwa na penati aliyosababisha Zawadi Mauya, "Sipendi kufungwa"

 Gamondi achukizwa na penati ya Zawadi Mauya,

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha mchezaji wake Zawadi Mauya kusababisha penati iliyozaa bao kwenye mchezo wao wa marudiano wa Klabu Bingwa dhidi ya ASAS FC ya nchini Djibouti.


Mchezo huo uliopigwa jana Agosti 26, 2023 katika Dimba la Azam Complex umemalizik kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 5-1 n kuwafanya Wananchi wafuzu hatua inayofuata ambapo watakutana na Al-Merreikh ya Sudan.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, Gamondi ambaye alionekana kuchukia wakati Mauya akisababisha penati hiyo, amewaponga wachezaji wake kwa mchezo mzuri huku akisema kuwa hakupendezwa na makosa yaliyofanywa na mchezaji wake kusababisha penati iliyozaa bao.


"Ninawapongeza wachezaji wangu kwa kujituma, mpango wetu ulikuwa kushanbulia na kupata mabao mengi na kweli tumefanikiwa. Nawapongeza mashabiki kwa kuendelea kutusapoti, pia ninawapongeza wapinzani wetu kwa changamoto waliotupatia, ASAS ni timu nzuri na wamecheza vizuri.


"Sijafurahishwa na namna ambavyo wachezaji wangu walifanya makosa na kusababisha penati, malengo yetu ilikuwa tusifungwe hata bao moja na hili tumekuwa tukilifanyia kazi kuanzia kwenye uwanja wa mazoezi.


"Hata kama tunaongoza kwa mabao mengi, nimewashawaambia sipendi waruhusu mabao kizembe, sipendi kufungwa fungwa. Nafahamu mpira ni mchezo wa makosa, huwezi kusema hutafungwa, tunajitahidi kuwapa mbinu wachezaji wetu wasifanye makosa kama haya.


"Kwa vile hili limetokea ni somo kwetu kwenda kuangalia mapungufu yalikuwa wapi na kurekebisha ili siku nyingine lisifanyike kosa kama hili. Huko mbele hatua zitakuwa ngumu na ukifanya kosa moja inaweza kuigharimu timu, kwa hito tutalifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi," amesema Gamondi.


Mauya aliingia kipindi cha pili dakika za mwishoni akichukua nafasi ya kiungo Jonas Gerald Mkude lakini wakati akiwa katika harakati za kukaba alicheza madhambi yaliyozaa bao la kufutia machozi kwa ASAS dakika ya 85.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz