Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Amesema Phiri hana maelewano mazuri na viongozi wa Klabu hiyo tangu alipoanza kudai maslahi yake kutokana na mkataba wake unavyosema kipindi anafanya vizuri.
Alikuja na akawa anafanya vizuri sana, anafunga mabao mengi, akapendwa na mashabiki, basi hapo akaanza kudai maslahi yake kutokana na mkataba wake unavyosema.
Bahati mbaya akapata majeraha ambayo yalimuweka nje, ndipo alipoibuka Jean Baleke akawa anafanya vizuri pia basi hapo viongozi ndipo wakaanza kupenyeza 'Vimemo' kwenda kwa kocha kwamba mpange Baleke achana na Phiri.
Makocha pia wanaokuja hapa licha ya kujifanya ni 'Professional' lakini huwa wanajali sana ugali wao, ada za watoto na kodi ya meza hivyo wanawasikiliza sana hawa viongozi wa hivi vilabu, kwani makocha wenye timu Dunianini wachache ukilinganisha na wasiokuwa na timu.
Hivyo wanamkomoa kutokumpa nafasi ya kucheza, nasikia pia Wakala wake alitaka kuvunja mkataba, ameseam Edo.
Post a Comment