Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama anatarajiwa kukosa mchezo wa nusu fainali wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida FG
Mchezo huo utapigwa Alhamisi, August 10 katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
Chama anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting msimu uliopita
Chama alikosa mechi dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union katika msimu uliopita na mechi ya nusu fainali dhidi ya Singida FG itakuwa ya mwisho
Licha ya kumkosa Chama, kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira hatakuwa na hofu yoyote kwani ana kikosi kipana chenye wachezaji bora zaidi ya mmoja katika kila nafasi
Luis Miquissone, Aubin Kramo, Willy Onana wote wanaweza kutumika katika nafasi ambayo hucheza Chama
Post a Comment