Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Arsenal imetwaa Ubingwa huo baada ya kuifunga Manchester City penati 4-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley, London.
Man City ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 77 kupitia kwa Cole Palmer kabla ya Leandro Trossard kusawadhisha dakika ya 90+11' na kufanya mchezo uende matuta ili kuamua nani awe bingwa.
Arsenal walifunga penati zao zote nne kupitia kwa Fabio Vieira, Martin Odegaard, Leandro Trossard na Bukayo Saka wakati Man City wakipata penati moja kupitia kwa Bernardo Silva huku Kevin De Bruyne na Rodri wakikosa.
Hii ni mara ya tatu Arsenal na Manchester City zinakutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii; Arsenal ilishinda michezo miwili iliyopita - Arsenal 4-0 Man City (1934) na Arsenal 3-0 Man City (2014).
Post a Comment