Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Gamondi amesema amewaandaa vijana wake vyema, watawaheshimu wapinzani wao lakini wamejipanga kucheza kandanda safi na kupata ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wao
"Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi, ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyumbani nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga"
Aidha Gamondi amebainisha kuwa baadhi ya wachezaji walipata changamoto ndogo ndogo katika mechi tatu zilizopita, baada ya mazoezi ya mwisho leo atafahamu wale ambao watakuwa tayari kwa mchezo huo
"Tumecheza mechi tatu katika kipindi cha siku 10, tunatumia uwanja wenye nyasi bandia ni wazi ziko changamoto ambazo wachezaji wetu wamepata. Sio utamaduni wangu kutangaza mchezaji gani atakuwepo na nani hatakuwepo"
"Muhimu ni kuwa hakutakuwa na mabadiliko katika mfumo wetu wa uchezaji, tutacheza kandanda safi, kuwa makini katika ulinzi, kutengeneza nafasi na kufunga mabao. Hatutajali idadi ya mabao ambayo tutafunga, jambo muhimu kwetu ni kupata ushindi," alisema Gamondi
Pamoja na kuanza mazoezi ya gym, kiungo mshambuliaji Skudu Makudubela hatakuwa sehemu ya mchezo huo
Gamondi amesema nyota huyo atajumuika kwenye mazoezi ya timu kuanzia Jumatano
Yanga inaweza kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kama itaibuka na ushindi mnono katika mchezo huo
Post a Comment