Alichokisema Kocha mkuu wa Yanga kuhusu mechi ya kesho dhidi ya Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hana wasiwasi wowote kuelekea mchezo wa fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Mkwakwani


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi amesema ameshiriki mechi nyingi za dabi hivyo mchezo huo hautakuwa tofauti


Aidha, kocha huyo raia wa Argentina amesema mchezo huo hautakuwa vita, anaamini ni mechi nzuri ya kuwapa furaha mashabiki


"Ni Furaha kwangu kucheza dabi kesho na haitakuwa na presha kwani nimeshakutana na dabi nyingi hapo kabla. Hii siyo vita ni mpira wa miguu, ukishinda au kufungwa maisha yanaendelea"


"Huu ni mchezo ambao majukumu yangu kama kocha sio makubwa sana, wachezaji wanafahamu wanacheza kwa ajili ya mashabiki wao ambao watajitokeza kwa wingi kuwashangalia. Nimesimamia dabi nyingi nikiwa Sundowns, Wydad, Raja, Etoile Sahel na nyingine"


"Ninatamani nicheze hata mechi 30 za msimu mzima dhidi ya Simba kwa sababu ni dabi ambayo wachezaji wako tayari wakati wowote kuicheza," alisema Gamondi


Mlinzi wa kati Dickson Job amesema maandalizi yamekamilika na wanasubiri siku ya kesho ifike ili waweze kushuka dimbani kuwapa furaha mashabiki wao

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post