Alicho kisema kocha wa Yanga baada ya kuipa kichapo Cha mbwa mwizi KMC - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kisema kocha wa Yanga baada ya kuipa kichapo Cha mbwa mwizi KMC

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kandanda safi katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya KMC


Jana katika uwanja wa Azam Complex, Yanga ilianza ligi kibabe kwa ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo ambao Wananchi walitakata kwa dakika zote 90


"Pointi tatu muhimu zinazotuongezea kujiamini, Tulionyesha tuko kwenye njia sahihi. Tulicheza kandanda la kuvutia, usisahau tulicheza dhidi ya timu nzuri sana"


"Walicheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza lakini tulikuwa bora sana na tuko fiti pia. Nafurahi kwa sababu ushindi huu umewapa furaha mashabiki wetu, huu ni aina ya mpira ambao nataka timu yangu icheze"


"Bado kuna mechi 29 nyingine. Tutacheza kama mabingwa lakini tutawaheshimu wapinzani wetu. Sisi ndio mabingwa watetezi hivyo kila timu inataka kutufunga. Bado tuna safari ndefu lakini huu ni ushindi muhimu sana," alisema Gamondi


Yanga itacheza mechi nyingine ya ligi kuu Augudt 29 dhidi ya JKT Tanzania mchezo huo pia utapigwa uwanja wa Azam Complex

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz