Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jana
Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo, Gamondi alisema walistahili ushindi huo kwa kuwa walikuwa bora zaidi kuliko wapinzani wao hasa katika kipindi cha pili
Gamondi alisema kipindi cha kwanza hawakucheza katika ubora wao, ni kutokana na huo kuwa mchezo wa kwanza wa kimashindano huku wakitoka kufanya mazoezi magumu ya pre-season
Gamondi pia hakufurahishwa na hali ya 'pitch' ya Mkwakwani, vijana wake hawakuwa huru kucheza soka lao
"Nawapongeza wachezaji wangu kwa kushinda mchezo huu. Tulitarajia mchezo ungekuwa mgumu kwa sababu huu ni mchezo wa kwanza wa mashindano msimu huu"
"Kipindi cha pili tulikuwa bora zaidi tulitengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wetu ambao hawakutengeneza nafasi yoyote. Kulikuwa na changamoto ya uwanja kwani haukuturuhusu kucheza vile tulivyotaka lakini jambo muhimu kwetu tumefunga mabao mawili na kusonga mbele hatua inayofuata"
Gamondi amesema kikosi chake kimesheheni wachezaji wazuri, zipo nyakati atafanya 'rotation' kwa kulingana na mechi zinazowakabili
Baadhi ya wachezaji hakuwatumia jana kwa kuwa hawakuwa tayari kutumika katika mchezo huo
Mshambuliaji Hafiz Konkoni na kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua waliushuhudia mchezo huo wakiwa jukwaani
Nyota hao walichelewa kujiunga na wenzao katika pre-season iliyofanyika Avic Town
Post a Comment