Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Tukio la Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kujiunga na Klabu ya SImba huku akikana hadharani kutowahi kuwa na kadi ya Uanachama ya Yanga SC yeye ni Simba damu damu, basi Haji Manara amemuibukia na kumtolea uvivu.
Manara ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga, amedai kuwa Kiba ameenda Simba ili akatoe burudani kwenye tamasha la Simba Day na atachangamsha damu kwa kila atakayekuwepo kwa hiyo siyo kitu kibaya.
Haji ambaye aliwahi kuwa Msemaji wa Simba, ameongezea kuwa, kitendo cha Alikiba kuihama Yanga kimemuumiza huku akisema anamjua vizuri yeye na Diamond Platnumz kuhusu mapenzi na ushabiki wao.
"Kwangu mimi sioni shida yoyote, watu wameleta mzigo akae nyumbani kufanyaje? Mwache aende akaburudishe, kwetus sisi hatupunguzii chochote wala hatuongezei chochote.
"Mambo ya kumkimbia Diamond mimi sifuatilii sana, sioni dhambi kwenye hilo ni kama fursa wala Wanayanga msimchukulie tofuati," amesema Manara.
Post a Comment