Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Dirisha la usajili la CAF litafungwa kesho Jumatatu, Julai 31 2023 habari njema kwa Wananchi ni kuwa timu yao imefunga usajili kwa wakati
Katika dirisha hili Yanga imesajili wachezaji nane pia ikiwapa mkono wa kwaheri baadhi ya wachezaji
Mshambuliaji Hafiz Konkoni alifunga usajili ambapo pia Yanga imewasajili nyota wa kigeni Gift Fred, Skudu, Pacome Zouzoua, Yao na Maxi Nzengeli
Jonas Mkude na Nickson Kibabage ni wachezaji pekee wa ndani waliosajiliwa katika dirisha hili
Wachezaji walioondoka ni Feisal Salum, Erick Johora, David Bryson, Djuma Shaban, Abdallah Shaibu na Mamadou Doumbia
Wengine ni Dickson Ambundo, Yannick Bangala, Tuisila Kisinda, Bernard Morrison na Fiston Mayele
Post a Comment