Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Shabiki kindakindaki wa Simba Sc, Mzee Mchachu amesema kuwa kutokana na usajili mkubwa wa wachezaji bora walioufanya msimu huu, mtani wao Yanga ajipange kuachia mataji yote aliyochukua msimu uliopita.
Mchachu amesema hayo mara baada ya kuona kikosi cha Simba kilichosajiriwa kinatia matumaini ya kurejea kwenye ufalme wao walioupoteza mbele ya Yanga kwa miaka miwili sasa.
"Mimi nawapa Simba asilimia 100 ya kuchukua Ubingwa mwaka huu, kwanza mtani atuache, tumewapa heshima miaka miwili, wamechukua ubingwa miaka miwili na wamechukua medali ya shirikisho.
"Lakini mwaka huu hawaingii hata makundi na mbaya zaidi mwaka huu wakitoka ndo wametoka hakuna cha kwenda shirikisho tena, ndiyo bye bye tena! Ni simba tu ndiyo ataweza kuingia makundi," amesema Mchachu.
Post a Comment