Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Msimu uliopita Yanga Princess haikufikia malengo yake licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye kikosi
Kuelekea msimu ujao, maboresho yameanza na benchi la ufundi kwani Haaulobono ni kocha mwenye uzoefu mkubwa katika kufundisha soka la Wanawake
Ameinoa klabu ya Green Buffalos ya Zambia kwa miaka 15 akiongoza timu hiyo ya Wanawake kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara 6 na taji la CECAFA
Haalubono pia ndiye Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia umri chini ya miaka 20
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji ambaye ni mlezi wa Yanga Princess alitoa ahadi kuwa watafanya maboresho zaidi kuelekea msimu ujao
"Msimu uliopita haukuwa mzuri licha maboresho makubwa tuliyofanya, sasa tunautumia kama changamoto, tutaimarisha mapungufu yote ili kuhakikisha msimu ujao Yanga Princess inatimiza malengo ya kutwaa ubingwa," alisema
Post a Comment