Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Leo huko kwenye mitandao ya kijamii kumeibuka tetesi kuwa kuna mchezaji amepokwa huko uwanja wa ndege akiwa ametua nchini kwa ajili ya kujiunga na Yanga
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesisitiza kauli yake aliyoitoa jana kuwa walishafunga usajili wa msimu huu hivyo kinachoendelea ni maigizo tu
"Tulijua haya yatatokea ndio maana tukasema mapema kuwa tumeshafunga usajili, wachezaji wote tuliowahitaji wameshasaini mikataba yao zoezi lililobaki ni kuwatambulisha tu"
"Leo usiku tutatambulisha mchezaji mmoja halafu hao wengine tutawatambulisha kwa utaratibu ambao tumeuandaa"
"Sisi hatununui wachezaji 'online', Wananchi watulie muda wa kushusha vyuma umekaribia," alisema Kamwe
Kiungo Fabrice Ngoma ndiye anayetajwa kutua nchini kujiunga na Simba, kumekuwa na mjadala kuwa ndiye namba sita ambaye Kamwe amekuwa akitamba nae kwa wiki kadhaa
Kamwe amesema Wananchi watulie namba sita wao yupo na watamtambulisha katika wakati mwafaka
Post a Comment