Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Straika wa Yanga Sc, Yusuph Athumani amejiunga na Klabu ya West Armenia ya nchini Armenia kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Yusuph amekamilisha dili hilo ikiwa ni siku chache baada ya kumalizana mkataba wake wa mkopo wa miezi sita kwenye Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambapo alikuwa na mchango mkubwa kwa ‘Wagosi wa Kaya’ kwenye kuvuna pointi zilizowasaidia kusalia Ligi Kuu.
Ikumbukwe Yusuph alijiunga na kikosi cha Young Africans akitokea katika Klabu ya Biashara United ya mkoani Mara, akiwa sehemu ya kikosi cha kihistoria cha Klabu hiyo kilichocheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.
Uongozi wa Young Africans Sports Club umeamtakia kila la kheri Yusuph Athumani katika kipindi chote atakachokuwa kwenye Klabu ya West Armenia.
Yusuph amekuwa mchezaji wa pili kutolewa kwa mkopo baada ya David Bryson aliyejiunga kwa mkopo pia wa mwaka mmoja kwenye Klabu ya JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.
Post a Comment