Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amewaaga Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo baada ya kujiunga na Pyramids Fc ya Misri
Mayele amewashukuru Wananchi kwa sapoti katika misimu miwili ambayo amecheza Tanzania
Amesema kwa ushirikiano wa viongozi, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki katika misimu miwili wameweza kushinda mataji yote ya ndani pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Mayele amebainisha kuwa haikuwa rahisi kwake kuondoka Yanga lakini ni wakati umefika wa kwenda kusaka changamoto sehemu nyingine
Amesema Yanga ni nyumbani, anaamini wakati mwingine atarejea na atapokelewa na kupewa sapoti kama aliyopata mwanzo
Post a Comment