Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wananchi wa Malawi wamepata bahati kwani watamshuhudia mchezaji mmoja aliyesajiliwa katika dirisha hili la usajili ambaye atajumuishwa katika kikosi kitakachosafiri kwanda Malawi siku ya Jumatano
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kesho Jumanne watamtambulisha mchezaji huyo ambaye anatarajiwa kuingia kambini na wachezaji wenzake tayari kwa safari
"Kutokana na heshima kubwa waliyotupa kwa kutualika katika sherehe kubwa za nchi, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ametoa zawadi kwa Wananchi wa Malawi kwa kumjumuisha mchezaji mmoja tuliyemsajili katika kikosi kitakachosafiri siku ya Jumatano"
"Mchezaji huyo tutamtangaza siku ya kesho, taarifa zaidi tutazitoa kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii," alisema Kamwe
Kamwe amebainisha kuwa Yanga imekamilisha michakato yote ya usajili, wachezaji wengine watatambulishwa baada ya zoezi la utambulisho wa jezi kukamilika
"Bado hatujafunga zoezi la Thank You kwani kuna wachezaji na watendaji wengine ndani ya klabu tutatangaza kuwapa mkono wa kwaheri lakini tumefunga zoezi la usajili"
"Tumewasajili wachezaji wote tuliowahitaji, kazi iliyobaki ni kuwatangaza tu. Tunaandaa utaratibu mzuri wa kuhakikisha klabu yetu inanufaika na utambulisho wa wachezaji hao," alisema Kamwe
Post a Comment