Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezaji huyo jina lake bado halijafahamika lakini jezi namba sita ambayo atakabidhiwa imepata umaarufu mkubwa na kuwafanya mashabiki kumsubiri kwa shauku kubwa
Jana katika uzinduzi wa wiki ya Mwananchi mkoani Mwanza, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema mchezaji huyo watamtangaza kwa utaratibu wa kipekee
Kamwe alibainisha kuwa nyota huyo na wenzake waliobaki, mpaka kufikia siku ya Jumanne watakuwa wametambulishwa wote
"Kama tulivyotangaza kuwa utambulisho wa wachezaji wetu umedhaminiwa na benki ya CRDB hivyo mchezaji namba sita atatambulishwa wa mwisho na tutazingatia haki za Mdhamini wetu"
"Bado hatujakamilisha utambulisho wa wachezaji wote, leo (jana) ilikuwa tutambulishe mchezaji mmoja hapa Mwanza lakini kutokana na changamoto za teknolojia tulikosa sceen kubwa ya kuweka hapa, bado hatujamaliza" alisema Kamwe
Yanga inatarajiwa kumtangaza mchezaji atakayekabidhiwa jezi namba sita usiku wa Jumanne (saa 6 na dakika 6) ambapo siku inayofuata atakuwa Makao Makuu ya benki ya CRDB
Wanachama na Mashabiki wa Yanga ambao watalipia kadi zao kupitia CRDB watapewa nafasi ya kupiga nae picha
Post a Comment