Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ametaka dakika 180 kuwapima vijana wake tayari kwa mikiki mikiki ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya awali ambayo itaanza mwezi August 2023
Yanga huenda ikamenyana na AS Vita katika moja ya mechi hizo ambazo zitapigwa Avic Town
Klabu ya AS Vita iko nchini Tanzani kwa ajili ya pre-season ambapo pia watacheza na Singida FG siku ya Jumatano ijayo kwenye Tamasha la Singida Day
Gamondi ameeleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs, hata hivyo amesema mechi hiyo haitaoshi kuwapima vijana wake kama wako tayari kwa msimu mpya
"Nahitaji mechi mbili ili kuona ubora na mapunguifu kwa wachezaji wangu mechi moja haiwezi kunipa mwanga wa kuamini kuwa nina timu nziri na ya ushindani, mbele nina mechi ngumu ambayo itaamua njia yangu ya kuanza kupata mataji"
"Usajili uliofanyika kila mmoja ameona, ila mechi moja iliyochezwa haiwezi kuwa na majibu sahihi ya kuona mwanga wa kikosi ambacho kinahitaji kutetea mataji ambayo tulishinda msimu uliopita," alisema
Post a Comment