Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amedokeza kuwa mchezaji anayetangazwa leo ni mchezaji bora (MVP) katika ligi anayotokea 2022-23
"Baada ya kumtambulisha Waziri a burudani, bado hatujamaliza, leo tunashusha chuma kingine. Ni mchezaji bora zaidi katika ligi anayotoka"
"Usajili tuliofanya umezingatia mahitaji ya timu yetu, Wananchi wajiandae kupokea chuma kingine leo," alitamba Kamwe
Kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua kutoka Asec Mimosas ndiye Wananchi wanasubiri kuthibitisha utambulisho wake
Zouzoua ndiye mchezaji bora wa kikosi cha Asec Mimosas katika msimu uliopita lakini pia ndiye mchezaji bora (MVP) wa ligi kuu ya Ivory Coast
Ni kama ilivyokuwa kwa Stephane Aziz Ki, ambaye alitua Yanga msimu uliopita akiwa MVP wa Ivory Coast
Zouzoua anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji lakini pia anamudu kucheza kama kiungo wa ukabaji
Hivi karibuni alizawadiwa gari na Taasisi ya kiungo wa FC Barcelona Frank Kessie baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Asec Mimosas na ligi kuu ya Ivory Coast
Katika msimu uliopita Zouzoua alifunga mabao saba na kutoa pasi nne za mabao
Post a Comment