Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Winga hatari wa Asec Mimosas Kramo Aubin anatajwa kuwa tayari amemalizana na mabosi wa Simba
Baada ya kuinasa saini ya Essomba Onana ambaye anamudu kucheza nafasi zote za winga, ujio wa Kramo unakwenda kuimarisha zaidi eneo hilo
Kibu Denis na Pape Ousmane Sakho watakuwa amepata washindani sahihi katika nafasi zao
Winga huyo anatumia miguu yote kwa ufasaha hivyo kumfanya kuwa mchezaji ambaye Simba inaweza kumtumia katika nafasi zote za winga na hata kiungo mshambuliaji
Ukizungumzia wachezaji waliong'ara katika kikosi cha Asec kilichocheza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita, Kramo ni miongoni mwao
Simba haikuanza kumfuatilia Kramo msimu huu, hata msimu uliopita alikuwa kwenye orosha ya nyota waliokuwa wakiwaniwa lakini mpango wa kumnasa haukufanikiwa
Katika dirisha hili la usajili, Simba imefanya maboresho katika kila eneo kuanzia mlinda lango, safu ya ulinzi, kiungo na safu ya ushambuliaji
Post a Comment