Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Jana baada ya klabu ya Simba kutangaza kuachana na Sawadogo ikiwa ni miezi sita tangu aliposajiliwa, Wanasimba walionekana kufurahia hatua hiyo
Ahmed amesema sio kitu kinachoweza kumfurahisha mchezaji pale anapoona mashabiki wanashangilia anapoachwa lakini jambo la msingi ni kuwa mashabiki wametuma ujumbe kwa viongozi wao juu ya nini wanataka
"Mashabiki wengi wa Simba wamefurahi kuondoka kwa Ismael Sawadogo Kama mchezaji inaumiza kuona watu wanafurahia kuondoka kwako na kwa kiongozi inaumiza kuona uliyemsajili amewapa furaha watu siku ya kuondoka"
"Sio kama wanamchukia ila hawakupata walichotaka kutoka kwake. Lakini furaha ya Wana Simba sio kuondoka kwa SawaD, Furaha yao ni kwa sababu wana matumaini atakuja mtu bora zaidi"
"Sawadogo ni top Class player kama angepata muda dunia ingemuona tena Yaya Toure akiwa na jezi nyekundu. Shida iliyopo wana Simba hawana muda wa kumsubiri mtu Wana Simba wanakimbia hivyo hawapo tayari kuongozana na mtu anaetembea"
"Haya ndio maisha ya Kibebari yalivyo, sasa tunaganga yajayo, Tunaleta mtu wa kumaliza shida za katika ya Uwanja Mchezaji ambae akikaa katikati anaugawa uwanja mara mbili yaani mpizani anaona golini kwetu mbali na washambuliaji wetu wanaona golini kwa mpinzani karibu"
"Kwa ufupi uyo mtu atakua anafanya Delivery anatoa mali sehemu moja kupeleka sehemu nyingine kwa uharaka na ubora," aliandika Ahmed kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Post a Comment