Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kipa namba moja wa Klabu ya Simba, Aishi Manula amesema kuwa hajaona umhimu wa kumshauri aliyekuwa mchezaji mwenzake, Jonas Mkude kuhusu kwenda Yanga kwani kila mchezaji anajua nini anakihitaji ili kutimiza malengo ya maisha yake.
Manula ameongeza kuwa, si jambo baya kwa mchezaji kuhama kutoka timu moja kwenda timu nyingine ndani ya nchi moja kwani hata Ulaya wachezaji wanafanya hivyo na soka ni biashara hivyo hata mchezaji anahama timu ili kutafuta maisha bora zaidi ama nafasi ya kucheza.
“Mtu akikwambia kutoka Simba kwenda Yanga ni usaliti basi huyo atakuwa na matatizo yake na hajui mpira. Tunaona wachezaji wanatoka Chelsea wanakwenda Arsena, wanatoka Arsenal wanakwenda Man United au kutoka man City kwenda Chelsea.
“Kama mchezaji anatoka klabu moja kwenda nyingine hapa nchini halafu shabiki anasema ni usaliti nakuwa sijui wanaangalia kwa namna ipi na wanamchukulia mchezaji ni nani kwao.
“Kama mchezaji ana urithi kwenye timu baada ya kumaliza carrier yake ya soka basi atakuwa msaliti kwenye hiyo timu. Kama leo nisema nahama ukoo wangu, hapo ndio usaliti kwa sababu nina urithi kwenye ukoo wangu.
“Kama mchezaji ana urithi kwenye hiyo timu baada ya kustaafu labda anapatiwa kiwanja cha klabu, lakini kama kuondoka kwenye hiyo timu anakuwa na maisha yake mengine, anapaswa kuangalia maisha yake kwa sababu baada ya huo mpira yeye ndio atakuwa anahangaika na maisha yake, watoto wake, kodi, umeme na mambo mengine ni yeye.
Post a Comment