Vigogo wa CAF watua Dar kufatilia jambo hili

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wakati Serikali ikitangaza bajeti ya Sh31 bilioni kukarabati Uwanja wa Mkapa, timu ya ukaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) wametua nchini jana kufanya ukaguzi wa utayari wa Tanzania kuandaa fainali za Mataifa Afrika (Afcon) 2027.


Tanzania kwa kushirikiana na Kenya pamoja na Uganda, zimeomba kuandaa fainali hizo ikishindana na Algeria, Botswana na Misri, ambazo nazo maombi yao yako mezani.


Gazeti hili linafahamu kuwa timu hiyo ya wakaguzi, ilianzia Kenya, kisha ikaelekea Uganda na jana limekuja Tanzania, ambako itakuwepo kwa siku zisizopungua tano, kukagua na kisha kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi ili kutimiza vigezo vya kupitishwa kuandaa fainali hizo.


Maeneo matano ambayo timu hiyo ya CAF itayafanyia ukaguzi ni Uwanja wa Ndege wa JNIA, viwanja vya mazoezi, viwanja vya mechi, hospitali pamoja na hoteli.


Kwa mujibu wa muongozo wa uandaaji wa mashindano hayo, uwanja wa ndege unapaswa kuwa katikati au jirani kwa umbali usiozidi kilomita 200 kutoka jiji/mji ambao mechi za mashindano hayo zitachezwa na kama ikishindikana, uwe na uhakika wa kuwepo na usafiri wa ndege wa kufikia maeneo hayo.


Kwa upande wa viwanja vya mechi na mazoezi, vinapaswa kutimiza vigezo vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) vya kuandaa mechi za kimataifa, ambavyo ni kuwa na chumba cha vipimo na matibabu, ukumbi wa mikutano, ukumbi wa vyombo vya habari na kadhalika.


Pia, hoteli zinapaswa kuwa zile za nyota tano, lakini pia hazipaswi kuwa umbali mrefu kutoka katika uwanja wa mechi na vile vya mazoezi vitakavyotumika na timu zilizopangwa katika mji/jiji husika.


Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alithibitisha ujio wa maofisa hao wa Caf na kile ambacho wanakuja kukifanya.


Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post