Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amesema ni mapendekezo ya kocha Miguel Gamondi baada ya kukifanyia tathmini kikosi chake
"Ni kweli kabla ya dirisha la usajili kufungwa, tutaleta mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kushirikiana na hawa waliopo. Kocha wetu (Gamondi) ameridhika na kila nafasi tuliyofanya maboresho lakini akapendekeza tuongeze nguvu katika eneo la ushambuliaji"
"Tuko kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo ambaye tunaamini ataendeleza burudani kwa Wananchi kwa kufunga mabao," alisema Kamwe
Dirisha la usajili CAF litafungwa Jumatatu, Julai 31 hivyo ni wazi Yanga inapaswa kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo kabla ya Jumatatu
Bado Yanga haijatangaza kumuuza mshambuliaji Fiston Mayele wakisubiri klabu iliyomsajili (Pyramids Fc) ikamilishe mchakato wote wa kumsajili
Post a Comment