Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Arafat amewataka Wanayanga waendelee kuwa na imani na uongozi wao chini ya Rais Injinia Hersi Said kwani malengo yao ni kuleta mafanikio zaidi Jangwani
Akizungumzia usajili, Arafat amewataka Wananchi kuwa na amani kwani muda sio mrefu watatangaziwa wachezaji waliosajiliwa kuongeza nguvu kikosini
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;
"Wiki kama hii mwaka Jana, wanachama wa Yanga walitumia haki yao ya kikatiba, waliniamini na kunichagua kuwa Makamu wa Rais klabu yetu pamoja na uongozi mzima wa Yanga. Julai 10, 2023 nimetimiza mwaka mmoja nikiwa Makamu wa Rais wa Yanga.
Natumia fursa hii kuwashukuru wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa imani kubwa mliyonayo kwangu na uongozi mzima uliopo madarakani.
Msimu uliopita (2022/23) ulikuwa ni msimu wetu wa kwanza madarakani, tumefanikiwa kushinda mataji yote tuliyoshiriki kwenye mashindano ya nyumbani lakini kwa upande wa mashindano ya kimataifa tumefika Fainali ya Kombe la Shirikisho na kumaliza katika nafasi ya pili.
Wananchi naomba muendelee kuniamini pamoja na uongozi mzima wa Yanga chini ya Rais wetu Injinia Hersi Said ili tuendelee kuipeleka klabu yetu kwenye mafanikio zaidi.
Ile Ahadi yetu iliobakia kwa timu zetu nyengine sasa wakati wake ndio umefika na tunakuja kuendeleza furaha Zaid.
Msitishwe na Wazee wa "Recycle Bin" vyuma vinashuka muda sio mrefu na ni vyuma kweli kweli na Mshindo Mmoja"
Post a Comment