Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ni Dhahir Uongozi wa Young Africans umekamilisha usajili wa Kiungo fundi kutoka Ivory Coast Zougrana Mohamed, ambaye pia ana uwezo wa kucheza eneo la ushambuliaji.
Dili la Zougrana Mohamed limefikia asilimia 99 akitokea klabu ya Asec Mimosas ambayo alitokea kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephanie Aziz Ki.
Zagrana alijiunga na Asec Mimosas, Agosti 2, 2021, ambapo bado ana mkataba wa mwaka mmoja ambao Young Africans wameununua na sasa wana uhakika wa kumtambulisha msimu ujao.
Taarifa kutoka Young Africans zinaeleza, wamekamilisha dili la Zougrana, ambaye anatajwa kuwa atapewa jezi namba 6 ambayo ilikuwa ikiwavliwa na kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye ametimkia Azam FC.
“Naomba nikuhakikishie kuwa ile kauli ya msemaji wetu kuwa jezi namba sita itavaliwa na fundi sana wa mpira basi amini kuwa fundi huyo ni Zougrana Mohamed, ambaye tayari tumeshakamilisha usajili wake,” kimesema chanzo hicho.
Young Africans kupitia Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said alizungumzia hilo la usajili kwa kusema: “Tumepanga kufanya usajili mkubwa, na hakuna mchezaji tutakayemshindwa kumsajili, kikubwa awepo katika mipango ya benchi la ufundi.”
Post a Comment