Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo wa Yanga Khalid Aucho amechelewa kurejea nchini kuungana na wenzake katika pre-season Avic Town kujiandaa na mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa Jumamosi, Julai 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kukosekana kwa Aucho kumeibua maswali miongoni mwa Wananchi, wengi wakitaka kufahamu alipo kiungo huyo tegemeo
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Aucho aliomba kwa uongozi apatiwe siku kadhaa ili ashughulikie masuala ya kifamilia
"Aucho anayo ruhusa ya uongozi, aliomba tumpatie siku chache aweze kushughulikia masuala ya kifamilia huko Uganda. Lakini jambo jema ni kuwa alipatiwa program zote za mazoezi ambayo wenzake wanafanya"
"Unajua mazoezi ya mwanzo kwenye pre-season yanahusisha kuimaisha mwili, pumzi na misuli zaidi, tunaamini amefanya mazoezi hayo na akirejea atakuwa sawa na wenzake, " alisema Kamwe
Yanga inaendelea kujifua Avic Town tayari kuikabili Kaizer Chiefs siku ya Jumamosi katika mchezo ambao mashabiki wa Yanga wataishuhudia timu yao mpya chini ya Kocha Miguel Gamondi na wachezaji wapya waliosajiliwa
Post a Comment