Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Yanga imeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya NMB Tanzania katika kuongeza ufanisi wa Usajili na Masuluhisho ya kifedha kwa Wanachama na Mashabiki
Makubaliano hayo yamesainiwa leo Makao Makuu ya benki ya NMB, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisaini kwa niaba ya klabu
Kwa makubaliano hayo, Mwanachama na Shabiki wa Yanga sasa anaweza kujipatia kadi yake katika Tawi lolote la NMB nchini Tanzania
Hii ina maana hata wale ambao wako mikoani na wilayani wanaweza kujipatia kadi zao katika Matawi ya NMB
Injinia Hersi amesema makubaliano hayo yatawaongezea wigo kwa Wanachama na Mashabiki wao kujisajili kwa urahisi
Makubaliano hayo pia yanakwenda mpaka kwenye eneo la miundombinu ambapo Yanga inatarajiwa kujenga uwanja wake eneo la Kaunda, NMB watakuwa washirika
Yanga pia itakwenda kusaini mkataba kama huo na benki ya CRDB
Post a Comment