Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu za Yanga, Simba, Azam Fc na Singida FG kukamilisha michakato yao ya usajili kwani dirisha la CAF linakaribia kufungwa
Dirisha hilo linatarajiwa kufungwa siku ya Jumatatu, Julai 31. Klabu zinazoshiriki Ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho zinapaswa kukamilisha usajili wake ndani ya muda huo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF, mpaka sasa Singida FG na Simba zimesajili wachezaji 29, Azam Fc imesajili wachezaji 25 huku Yanga ikiwa imesajili wachezaji 24
Yanga na Simba zitashiriki ligi ya mabingwa wakati Azam Fc na Singida FG zitashiriki kombe la Shirikisho
Kila timu inaruhusiwa kusajili hadi wachezaji 40 kwa ajili ya mashindano ya CAF
Post a Comment