Soko la usajili lamdodea Harry Maguire

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Manchester United inakumbana na ugumu katika kumpiga bei Harry Maguire kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wa beki hjuyo wa kati wa kutoka England, imeelezwa.


Man United inahitaji kuuza baadhi ya mastaa ili kuongeza bajeti ya usajili dirisha hili. Lakini, baada ya kumaliza nafasi ya tatu Ligi Kuu England msimu uliopita na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hapo ndipo unapoibuka ugumu wa kumuuza Maguire.


Kwenye mkataba wa Maguire kuna kipengele kinafichua endapo timu itapata mafanikio ya aina hiyo, basi atalazimika kuongezewa mshahara.


Na hapo ugumu unakuja kwamba ili aondoke atalazimika kupunguza mshahara kitu ambacho kinawapa ugumu mabosi wa Man United kumshawishi beki huyo.


Maguire, 30, mkataba wake utafika tamati 2025 na kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja. Ripoti zinadai beki huyo yupo kwenye rada za klabu za West Ham, Tottenham na Newcastle. Man United walimsajili kwa Pauni 80 milioni kutoka Leicester City 2019.


Lakini, sasa wapo tayari kumuuza kwa bei ndogo baada ya kupoteza nafasi kikosi cha kwanza chini ya kocha Erik ten Hag.


Maguire alicheza mechi 31 msimu uliopita na nane kati ya hizo, ndizo alizoanzishwa kwenye Ligi Kuu England.


Wachezaji wengine wa Man United wanaoweza kuuzwa dirisha hili ni Fred, Donny van de Beek, Anthony Elanga na Dean Henderson, huku Jadon Sancho akihusishwa na Borussia Dortmund.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post