Simba yafanya maamuzi magumu kwa Chama na Saido

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama na Shomary Kapombe walikuwa wakila bata makwao kipindi hiki cha mapumziko, lakini ghafla wakapigiwa simu na mabosi wao na kutakiwa kukatisha likizo hizo na fasta watue jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa michuano.


Sio Chama na Saido tu, bali hata wachezaji wengine 21 wa kikosi cha sasa cha timu hiyo wakiwamo kipa Aishi Manula anayejiuguza kwao mjini Morogoro naye ametakiwa kufika Dar kama ilivyo kwa Kibu Denis, Shomary Kapombe, Habib Kyombo na John Bocco.


Nyota hao wa Simba wameitwa na mabosi hao kwa ajili ya vipimo vya afya watakavyochukuliwa kuanzia kesho kwa kundi la wachezaji wazawa kabla ya kuhamia kwa wageni, kisha kufuata nyota wale waliosajiliwa na kikosi hicho akiwamo Leandre Willy Onana Essomba aliyetoka Rayon Sports.


Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, mabosi wa Simba wameamua kuwaita wachezaji wote ili kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya safari ya nje ya nchi zikitajwa Afrika Kusini au Uturuki itakapowekwa kambi ya maandalizi ya msimu mpya kulingana na maelekezo ya Roberto Oliveira.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post