Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba ilielezwa kufuatilia saini ya Miquisonne kwa muda mrefu sana kwani tangu msimu uliomalizika ambapo mchezaji huyo hakua akipata nafasi ndani ya klabu yake ya Al-Ahly lakini hawakufanikiwa kunasa saini yake.
Luis Miquisonne alikua anasumbuana na wekundu wa Msimbazi kwenye suala la malipo ya mshahara wake ambao ulielezwa kua juu sana jambo ambalo mpaka sasa inaonekana wamekubaliana katika suala hilo na ndio maana mchezaji huyo anasubiri tu kutangazwa.
Simba wanaelezwa kupania usajili wa dirisha hili kuelekea msimu ujao ambao inaelezwa wamedhamiria kurudi kwenye ubora wao na kutwaa ubingwa wa NBC msimu ujao ambao wameukosa misimu miwili mfululizo mbele ya watani zao Yanga.
Wekundu wa Msimbazi mpaka sasa wamefanya sajili kadhaa ambazo zinaonesha wamedhamiria kwa kiwango kikubwa kurudisha ubora wao kwani wamesajili wachezaji wawili ambao wamekua wachezaji bora kwenye ligi zao walizotoka hii inatosha kuonesha Simba wanataka kuurudiaha ubingwa kwenye mitaa ya msimbazi.
Post a Comment