Simba watangaza kuweka kambi Uturuki - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba watangaza kuweka kambi Uturuki

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamegangaza kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya 2023-24.


Simba wametangaza suala hilo leo Julai 3, 2023 kupitia Simba App ambapo wameweka wazi kuwa kikosi kinatarajia kuweka kambi nchini humo kwa wiki tatu kabla ya kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.


Wamesema wakiwa nchini humo, wanatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki ambapo kikosi cha Simba kikiongozwa na kocha Mkuu Roberto Oliviera pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa na wale wa zamani, kwa pamoja watapata utulivu wa kupeana mbinu mpya kisha kurejea nchini.


Mapema hii leo, kundi la kwanza la wachezaji 12 wa Simba walifanya vipimo vya afya huku ikielezwa kundi la pili linatataji kufanya vipimo hapo kesho.


Wachezaji waliofanya vipimo jana ni pamoja na Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr', Mzamiru Yassin, Israel Mwenda na Shomari Kapombe.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz