Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kubwa zaidi na la kushangaza ambalo halijawahi kutokea ni kuwa Simba itazindua jezi hiyo katika kilele cha Mlima mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro.
Akizungumza leo Julai 15, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Imani Kajula amesema
"Nawambia rasmi hapa kwamba jezi ya Simba itazinduliwa juu ya Mlima Kilimanjaro
Jezi itaanza kupandishwa mlimani siku ya Jumatano na watakuwa kileleni siku ya Ijumaa na Jumamosi jezi itakuwa kwenye maduka yote nchini."
"Ijumaa saa 1:00 usiku jezi itakuwa imefika kileleni kwenye Mlima Kilimanjaro. Itazinduliwa na itaonekana rasmi siku hiyo."
Kauli hiyo kutoka kwa Klabu ya Simba inashusha presha kwa Mashabiki waliokuwa wanataka kujua tarehe rasmi ya upatikanaji wa jezi za Simba.
Post a Comment