Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba SC huwenda wakamtema mchezaji mmoja wa Kimataifa kwani mpaka sasa idadi ya wachezaji wa kigeni waliowasajili imevuka kiwango kinachoelekezwa na TFF.
Sheria inasema, timu inatakiwa kuwa na wachezaji kumi na mbili wa kigeni wakati Simba kwa sasa inao nyota 13 wa Kigeni ambao ni;
Che Fondoh, Willy Onana, Aubin Kramo, Fabrice Ngoma, Clotus Chama, Jean Baleke, Sadio Kanoute, Peter Banda, Henock Inonga, Said Ntibanzokiza, Moses Phiri, Luis Miquisson na golikipa Luis Jefferson.
Hapo kuna mawili, Simba wanaweza wasimpe thank you yeyote isipokuwa watamchagua mchezaji mmoja ambaye hatacheza ligi ya ndani akacheza michuano ya Kimataifa pekee au wakaamua kumpa thank you mchezaji wao mmoja.
Post a Comment