Simba kutangaza mchezaji mpya Leo Jumapili

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Jana ilikuwa siku ya mapumziko, Simba haikutangaza usajili wa mchezaji mpya zaidi ya kuthibtisha kuondoka kwa beki Joash Onyango ambaye amejiunga na Singida FG kwa mkopo wa msimu mzima


Leo saa 7 mchana Simba inatarajiwa kutambulisha usajili wake wa tatu baada ya Willy Essomba Onana na Aubin Kramo


Wanasimba wako tayari kumpokea nyota mwingine wa kigeni ambaye anakuja kuongeza nguvu katika kikosi cha kocha Robertinho Oliveira


Simba imemaliza kutambulisha safu ya ushambuliaji na sasa wanahamia kwenye safu ya ulinzi na kiungo


Nafasi ambazo bado zinasubiri nyota wapya ni golikipa, mlinzi wa kushoto, beki wa kati na kiungo mkabaji


Je leo ni zamu ya beki la Kimataifa Che Fondoh Malone kutoka Cotton Sport ya Cameroon au ni kiungo namba sita fundi wa mpira Fabrice Ngoma?


Au litakuwa lile kipa kutoka Brazil ambalo limetua na kocha Robertinho Oliveira? 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post