Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Tamasha kubwa zaidi la soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati SIMBA DAY litafanyika August 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema awali Tamasha hilo lilipaswa kufanyika August 08 lakini wamerudisha nyuma kwa siku mbili kutokana na ratiba ya Ngao ya Jamii
"Simba Day itakuwa Agosti 6, tumeirudisha nyuma siku mbili sababu Agosti 10 tutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii hivyo tunataka wachezaji wetu wapate muda wa kupumzika," alisema Ahmed
Wiki ya Simba inatarajiwa kuanza August 01 ambapo Wanasimba watashiriki matukio mbalimbali ya kujitolea kwenye jamii
Kikosi cha Simba kiko nchini Uturuki kikiendelea na maandalizi ambapo timu itarejea mwanzoni mwa mwezi August
Post a Comment