Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wananchi wote leo Wanakutana uwanja wa Benjamin Mkapa katika kilele cha wiki ya Mwananchi
Hii ni siku maalum kwa wanafamilia ya Yanga, kuukaribisha msimu mpya kwa kufurahi pamoja
Kutakuwa na burudani za kila aina uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 4 asubuhi
Mechi za kirafiki za timu ya vijana, wanawake, wakongwe na viongozi wa Yanga dhidi ya Wasanii zitapigwa
Burudani kutoka kwa wasanii wakubwa nchini, hii leo wasanii wote wakubwa hapa Tanzania watakuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa
Utambulisho wa kikosi kwa ajili ya 2023/24 utafanyika na kisha kufuatiwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs, saa 1 usiku
Hili ni siku ya furaha, siku ya mashabiki wa Yanga kufurahi pamoja na timu yao..!
Post a Comment