Sh mil 400 zamshusha mrithi wa Mayele Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Imeelezwa kuwa, Klabu ya Yaoundé kutoka nchini Cameroon, imeweka ofa ya dola 165,000 (Sawa na Sh 402,375,600 za Kitanzania) ili wamuachie mshambuliaji wao, Emmanuel Mahop anayetakiwa na Yanga.


Yanga inataka kumsajili mshambuliaji huyo ili awe mrithi wa Fiston Mayele aliyetimkia Pyramids FC ya nchini Misri kwa uhamisho wa shilingi bilioni 2.8.


Mahop ndiye mshambuliaji anayepewa nafasi kubwa ya kusajiliwa na Yanga kuelekea msimu ujao ambapo timu hiyo, inakwenda kucheza michuano Ligi ya Mabingwa Afrika, huku ikiwa na kazi kubwa ya kutetea mataji yake ya ndani ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo TanzaniaWeb imezipata, mshambuliaji huyo amerejea nyumbani kwao Cameroon kuendelea na majukumu mengine, huku akimbakisha meneja wake jijini Dar es Salaam kwa ajii ya kukamilisha dili lake.


Mtoa taarifa huyo alisema mazungumzo kati ya uongozi wa Yanga na klabu yake anayoichezea yamefikia pazuri sambamba na kutajiwa ofa ya dau la zaidi ya shilingi milioni 400 ili wauvunje mkataba wa mwaka mmoja ambao ameubakisha huko.


Aliongeza kuwa, hivi sasa mazungumzo ya maslahi binafsi ndiyo yanaendelea kati ya mchezaji na Yanga ikiwemo mshahara na mahitaji mengine kabla ya kusaini mkataba yakiwa chini ya meneja wa mshambuliaji huyo aliyekuwepo nchini kabla ya juzi Jumatatu kurejea kwao Cameroon.


“Mahop alikuwa hapa nchini kwa siku mbili, Jumapili na Jumatatu kabla ya jana Jumanne kurejea kwao na kumuacha meneja wake ambaye anaendelea na mazungumzo ya mwisho ya maslahi binafsi kati yake na viongozi wa Yanga.


“Mazungumzo yanakwenda vizuri hivi sasa ya kumsajili Mahop, hivyo kilichobaki ni Yanga kuwapa dau la usajili ambalo klabu yake inayommiliki wamewatajia ambalo ni kama Sh 400Mil ili wamuachie.


“Sasa hivi wanavutana katika mshahara pekee ambao ni mkubwa, uongozi wa Yanga unaendelea na mazungumzo naye ili wapunguze, na wampe mkataba wa miaka miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.


Yanga kupitia Rais wake, Injinia Hersi Said, alizungumzia hilo la usajili kwa kusema: “Licha ya kutangaza wachezaji wetu wapya tutakaowatumia msimu ujao, lakini bado hatujamaliza kufanya usajili, wapo wachezaji tutakaowatambulisha hivi karibuni.”

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post