Sasa tumekamilika, tukutane uwanjani - Robertinho

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Simba jana iliendelea kuwapa raha mashabiki wake kwa kutambulisha chuma kingine kipya, Che Fondoh Malone huku kocha mkuu Robertinho Oliveira aliyerejea juzi mchana akisema kwa majembe yaliyosajiliwa kikosi sasa kimekamilika


Kocha huyo Mbrazili alisema amekoshwa sana na namna mabosi wa Simba walivyotekeleza mapendekezo yako kwenye usajili kwani umeifanya timu hiyo ienee kila idara kwa sasa na kumpa jeuri ya kuamini atasumbua sana kwenye msimu ujao mbele ya wapinzani wao 


Robertinho anaamini kwa usajili uliofanyika, heshima ya klabu inarudi tena baada ya kumaliza misimu miwili mfululizo bila kutwaa taji lolote


Simba imeshawatangaza mawinga wawili wapya, Leandre Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda na Aubin Kramo aliyekuwa Asec Mimosas ya Ivory Coast najana imemtambulisha beki wa kati, Che Fondoh Malone kutoka Coton Sport ya Cameroon


Mbali na hao pia Simba inahusishwa kumalizana na kiungo Fabrice Ngoma aliyekuwa Al Hilal ya Sudan sambamba na kipa Mbrazili, Caique Luiz Santos


Mbali na nyota hao wapya, lakini Simba imebakiza baadhi ya majembe yake ya kikosi cha kwanza na ilikuwa inamalizana na wachezaji kadhaa wazawa wa kuchukua nafasi za waliotemwa hivi karibuni akiwamo, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, kipa Beno Kakolanya, Habib Kyombo anayetolewa kwa mkopo Singida Big Stars sambamba na Mkenya Joash Onyango


Kutokana na hilo kocha Robertinho alisema kilichotokea msimu uliopita wamekifanya chachu ya kuona kwa namna gani wanaweza kurejea msimu ujao wakiwa bora zaidi, hivyo iliwabidi kuingia sokoni na kusaka vifaa vya maana


"Kuifanya Simba kuwa mbali kiushindani na klabu zote kwenye ligi ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu, tunataka kutengeneza gepu kubwa kati yetu na wao ndio maana tumesajili wachezaji ambao wataongeza upana na ubora kwenye kikosi chetu"


"Ufinyu wa kikosi msimu uliopita ulikuwa ukituumiza, tulikuwa na michezo ambayo tulihitaji mabadiliko lakini utofauti wa ubora wa wachezaji ulitufanya kushindwa kupata tulichotaka."


"Ninayo furaha na utambulisho wa wachezaji, kwani nilikuwa najulishwa kila kilichokuwa kikifanyika, viongozi wamefanya kazi kubwa sasa ni wakati wetu wa kujiandaa na kutafuta uwiano mzuri wa uchezaji kama timu," alisema


Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post