Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Taarifa za uhakika ni kuwa klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati Che Fondoh Malone kutoka klabu ya Cotton Sport
Simba imekuwa kwenye majadiliano ya takribani wiki nzima na Cotton Sport juu ya uhamisho wa beki huyo mahiri ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Cameroon kilichoshiriki michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani
Malone alicheza mechi zote za Cotton Sport katika ligi ya mabingwa msimu uliopita, timu hiyo ikiwa kundi moja na Mamelodi Sundown, Al Ahly na Al Hilal
Huu ni usajili wa gharama kubwa ambao kwa hakika unaakisi malengo ya klabu ya Simba msimu ujao
Wanamsimbazi wanasubiri kwa hamu utambulisho wake ambao hakuna shaka utatokea!
Post a Comment